Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:14

Ethiopia yapinga kuandaliwa kikao kuhusu haki za kibinadamu nchini humo


Mpiganaji wa Tigray
Mpiganaji wa Tigray

Serikali ya Ethiopia imeukataa mpango wa baraza la haki za kibinadamu la umoja wa mataifa, wa kuandaa kikao maalum ijumaa wiki hii, kujadili hali ya kibinadamu nchini humo.

Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema kwamba imesikitishwa na kuhuzuniswa na uamuzi wa baraza la haki za kibinadamu la umoja wa mataifa, kuandaa kikao hicho baada ya kuombwa na umoja wa ulaya.

Serikali ya Ethiopia imezitaka nchi wanachama wa baraza hilo la umoja wa mataifa kukataa na kupiga kura kupinga kikao hicho.

Katika taarifa, serikali ya Ethiopia imesema kwamba kile ambacho baraza hilo ingefanya kwa haraka, ni kufanya uchunguzi kuhusu madai ya ukandamizaji wa haki za kibinadamu na unyama ambao umefanywa na kundi la wapiganaji wa Tigray TPLF, katika mikoa ya Afar na Amhara.

Baraza hilo la umoja wa mataifa limesema kwamba litajadili hali mbaya ya kibinadamu nchini Ethiopia.

Mwishoni mwa mwezi Novemba, Ethiopia ilitangaza kwamba ilikuwa imeunda tume maalum kusimamia madai ya ukandamizaji wa haki za kibinadamu wakati wa vita vinavyoendelea kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa TPLF, kaskazini mwa nchi hiyo

Serikali ilisema tume hiyo iliundwa kufuatia makubaliano kati ya tume ya haki za kibinadamu ya Ethiopia na ofisi ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa.

XS
SM
MD
LG