Janga la corona limesababisha mambo menage kusitishwa katika kila pembe ya dunia ikiwa ni pamoja michezo na mashindano mbali mbali. Hali hiyo imesababisha baadhi ya wachezaji na mameneja walioambukizwa virusi hivyo kujitenga na timu zao wakati wanapokea matibabu. Miongoni mwa wachezaji maarufu walioambukizwa ni mchezaji wa Juventus' Cristiano Ronaldo na Neymar wa PSG.
Wachezaji wa kimataifa wa kandanda wanaogua COVID-19
Mambukizo ya virusi vya corona yakiingia katika awamu ya pili kwenye nchi nyingi za dunia, kuna baadhi ya wachezaji mashuhuri wa kandanda wanaougua ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi hivyo.

1
Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan akishangilia goli alilofunga dhidi ya Bologna wakati wa michuano ya kundi A kati ya AC Milan na Bologna katika uwanja wa San Siro, mjini Milan, Italy, Jumatatu, Septemba 21, 2020.(AP Photo/Antonio Calanni)
Mshambuliaji wa timu ya AC Millan Zlatan Ibrahimovic aliambukizwa na virusi vya corona mwezi Septemba akisema,"COVID ilithubutu kumletea changamoto. Wazo baya." Alipona kutokana na maambukizo hayo wakati muda umefika wa pambano la Inter Milan huko Derby della Madonnia Oktoba 17.

2
Mchezaji bora wa dunia kwa miaka mitano Ronaldo akichezea timu yake iliyotoka sare 0-0 katika mchuano na Ufaransa wakati wa ligi ya Mataifa.
Cristiano Ronaldo, Juventus - Mshambuliaji - upande wa kushoto
Cristiano Ronaldo, mmoja wa nyota wakubwa wa kandanda duniani na ni miongoni mwa wanariadha maarufu zaidi, ameambukizwa virusi vya corona, Shirikisho la taifa la mpira wa miguu Ureno limetangaza Octoba 13. Mchezaji huyo mwenye umri wa maika 35 anaendelea vizuri na hana dalili za COVID-19 kwa mujibu wa Shrikisho hilo.

3
Kylian Mbappe wa Ufaransa akiutuliza mpira wakati wa mechi ya mpira wa miguu ya Ligi ya mataifa UEFA kati ya Croatia na Ufaransa kwenye uwanja wa Zagreb, Croatia, Jumatano, Octoba 14, 2020. (AP Photo/Darko Bandic)
Kylian Mbappe, PSG- Mshambuliaji - mfungaji magoli
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ufaransa (FFF) limethibitisha mapema Septemba Saint-Germain wa Paris na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe ameambukizwa COVID-19. Mbappe alitangaza kupona kwake na kurudu kucheza akifunga goli katika mchuano dhidi ya Nice wa mbao 3-0.

4
Neymar wa PSG wakati wa mchuano ya Ligi ya Ufaransa kati ya Paris Saint-Germain na Marseille katika uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Ufaransa, Jumapili, Septemba 13, 2020.(AP Photo/Michel Euler)
Mchezaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar ni moja kati ya wachezaji kadhaa wa Paris Saint-Germain aliyeambukizwa COVID-19, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali. Neymar alipona na yuko katika mafunzo na timu yake PSG kuanzia katikati ya mwezi Septemba.