Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 14:40

Uganda : Wabunge wa NRM wapinga Museveni kuwa rais wa maisha


FILE PHOTO: Ugandan President Yoweri Museveni attends an African Union summit in Addis Ababa, Ethiopia, Jan. 28, 2018.

Kundi la wabunge wa chama kinachotawala nchini Uganda, NRM, limeanzisha kampeni kupinga uamuzi wa juu wa chama wa kumtangaza rais Yoweri Museveni kuwa mgombea pekee wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021, na katika chaguzi zote zijazo kwa muda wa miaka 50.

Wabunge hao wamesema wanajitayarisha kuwasilisha shauri hilo mahakamani kupinga uamuzi huo.

Kundi hilo la wabunge wanaojulikana kwa kukosoa maamuzi ya chama yenye upendeleo kwa Museveni, na kuitwa wasaliti au waasi na wabunge watiifu kwa Museveni.

Waeleza kuwa maamuzi ya uongozi wa juu wa NRM wa kumuidhinisha Museveni kama mgombea pekee wa uchaguzi wa urais mwaka 2021 na katika chaguzi zitakazofuatia kwa muda miaka 50 ijayo, ni kinyume cha sheria, yenye kukosa muelekeo na ni kujitakia makuu.

Wabunge Theodore Ssekikubo, Patrick Nsamba, John Baptist Nambeshe, Gaffa Mbwatekamwa, Dr Sam Lyomoki na Monica Amoding wanaamini kwamba uamuzi huo umechukuliwa kuminya demokrasia ndani ya chama na kuwanyamazisha wote wenye nia ya kuchuana na Museveni kwa tiketi ya chama tawala katika uchaguzi mkuu.

Mbunge Amoding anasema kwa sababu yoyote ile, hakuna anayestahili kuwaambia raia wa Uganda kwamba Museveni ndiye kiongozi pekee anayejua changamoto za nchi hii ambazo inapitia na jinsi ya kutafuta ufumbuzi. Kizazi hiki kina watu wengi wenye uwezo wa kuongoza taifa hili vyema kabisa.

Kundi la wabunge wa chama hicho tawala, wanamsimamo kwamba kuwazuia wanachama wengine kugombea tiketi ya chama sawa na rais Museveni, ni dhihirisho tosha la ulafi wa madaraka na inavunja katiba ya chama. Sam lyomoki ni mbunge anayewakilisha wanawake katika bunge la Uganda.

Hata kama mlitaka mtu mmoja, muitishe uchaguzi halafu mseme hakuna aliyejitokeza ndipo mmtangaze huyu mtu mmoja. Huwezi simama tu katika mkutano wa uongozi wa chama na useme tumemtangaza Museveni kuwa mgombea bilakupingwa. Hiyo ni kinyume cha sheria, alisema Mbunge Lyomoki Sam.

Kando na kumuidhinisha Museveni mwenye umri wa miaka 74 na ambaye ametawala Uganda tangu mwaka 1986, kuendelea kugombea urais katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa muda wa miaka 50 ijayo tangu atakapopendekeza mrithi wake, uongozi wa juu wa NRM pia unataka upigaji kura kwa njia ya siri katika chama kufutiliwa mbali.

Chama cha NRM, kinataka wapiga kura kupanga foleni nyuma ya mgombea wakati wa uchaguzi wa mchujo kupitishwa na chama kuwania nafasi mbali mbali katika uchaguzi mkuu. Wabunge wanasema hatua hii inalenga kuwatisha wapiga kura na kueneza ubaguzi ndani ya chama.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Kennes Bwire, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG