Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 19, 2025 Local time: 17:44

Waandamanaji zaidi ya 100 Cuba wahukumiwa kutumikia kifungo

FILE - María Carla Milan Ramos akionyesha ndugu zake waliohukumiwa kifungo kwa tuhuma za kushiriki katika maandamanao yaliyokuwa yanapinga serikali, wakiwa nyumbani kwao huko La Guinera karibu na Havana, Cuba, (AP Photo/Ramon Espinosa, File)

Mahakama maalum nchini Cuba imewahukumu zaidi ya watu mia moja kifungo cha kati ya miaka 6 na 30 gerezani.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya watu hao kupatikana na makosa ya kushiriki maandamano ya kuipinga serikali, mwaka 2021.

Waandamanaji 128 wamehukumiwa kwa madai ya kuvuruga utulivu na kuharibu mali. Mtu mmoja ameachiliwa huru.

Kulingana na maafisa wa serikali waliohukumiwa walishiriki maandamano tarehe 11 na 12 mwezi July, katika manispaa mbili za mji mkuu, ambapo walipindua magari madogo kadhaa na kuwarushia vitu maafisa wa polisi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG