Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 00:46

Cuba yazindua kituo kuhifadhi kazi ya maandishi ya Fidel Castro


Rais wa Cuba Fidel Castro akiwa na ndugu yake Raul Castro (kushoto) [Maktaba]

Cuba imezindua kituo cha kuhifadhi kazi ya maandishi na kazi za kiongozi wa mapinduzi wa nchi hiyo Fidel Castro, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 5 tangu kifo chake.

Kituo hicho Fidel Castro Ruz, katika mji mkuu wa Havana, ni cha kwanza na cha kipekee kupewa jina lake.

Sheria ilipitishwa mwezi mmoja baada ya kifo chake mwaka 2016, iliyopiga marufuku taasisi mbalimbali, bustani, barabara na sehemu nyingine za umma kupewa jina la rais huyo na kiongozi wa chama cha kikomunisti.

Sheria hiyo ilipitishwa kutokana na ombi la Castro. Hata hivyo, haijazuia watu nchini humo kutengeneza sanamu yake na mabango kwenye mji wa Havana kama njia ya kumuenzi na kumpa heshima.

Castro aliongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa dikteta Fulgencio Batista mwaka 1959 na amesifiwa kwa kuunda mfumo wa utoaji huduma za afya na elimu kwa wote bila malipo.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la AFP

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG