Akizungumza na kituo kimoja cha habari, Jumatano, kiongozi huyo wa Cuba pia alishutumu mitandao ya kijamii kwa kuchochea maandamano hayo na kusema serikali ya Marekani ilikuwa ikichochea ghasia hizo katika azma yake ya kukomesha mapinduzi ya Cuba.
Rais wa Cuba anaeleza : "Jinsi wanavyotumia internet kwa sasa na jinsi wanavyotumia mitandao ya kijamii ni jambo la kutisha. Inawatenganisha watu. Inaleta uchungu na uongo mwingi, na nadhani ni kielelezo cha ugaidi wa vyombo vya habari.
Katika nchi za Amerika ya Kati, maandamano yamekuwa yakiendelea. Huko Argentina, vyama vya siasa vya mrengo wa kushoto vya Colombia, viliitetea serikali ya Cuba, na kukosoa vikwazo vilivyowekwa na Marekani na nchi nyingine dhidi ya nchi hiyo na kutetea kile walichokiita “ushahidi wa utawala wa ujamaa.”
Kwa upande mwingine, vikundi vinavyoipinga serikali viliishutumu, kwa kupotea kwa wafungwa wa kisiasa, na ukosefu wa uhuru wa kujieleza.
Cuba inakabiliwa na mzozo mbaya zaidi kwa miaka mingi, pamoja na athari ya janga la Corona, ambalo limezorotesha uchumi, utepetevu baina ya wafanyakazi wa serikali, na matokeo ya vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani, kushinikiza mabadiliko katika mfumo wa siasa.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali na AP