Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:35

Afrika kusini kuongeza wanajeshi 25,000 kupambana na ghasia


Wanajeshi wakiwa nje ya eneo la maduka huko Vosloorus, mashariki mwa Johannesburg, Afrika kusini, July 14, 2021.
Wanajeshi wakiwa nje ya eneo la maduka huko Vosloorus, mashariki mwa Johannesburg, Afrika kusini, July 14, 2021.

Afrika Kusini ilikusanya wanajeshi wake wa akiba  Alhamisi kwa lengo la kuzima  uporaji ambao umeharibu usambazaji wa chakula na vitu vingine

Afrika Kusini ilikusanya wanajeshi wake wa akiba Alhamisi kwa lengo la kuzima uporaji ambao umeharibu usambazaji wa chakula na vitu vingine muhimu na kusababisha pigo kubwa kwa uchumi wake.

Wanajeshi wote wa akiba wanapaswa kuripoti kazini mapema asubuhi Julai 15 katika vitengo vyao, mkuu wa jeshi Luteni-Jenerali Lawrence Mbatha alisema katika maagizo yaliyotolewa usiku wakati machafuko hayo yakiingia siku ya sita.

Askari wanapaswa kuripoti tayari na vifaa vyao muhimu, wizara ya ulinzi ilisema katika taarifa.

Siku ya Jumatano, serikali ilisema itawaita wanajeshi karibu 25,000 kwenda kukabiliana na hali ya dharura mara 10 ya idadi ambayo ilipeleka hapo awali.

Usumbufu huo umekata minyororo ya ugavi na usafirishaji, na kuharibu usafirishaji wa chakula, mafuta, dawa na vitu vingine muhimu.

Siku ya Jumatano, Waziri wa Ulinzi Nosiviwe Mapisa-Nqakula aliliambia bunge kwamba alikuwa amewasilisha ombi la kuongeza wanajeshi wasiopungua 25,000.

XS
SM
MD
LG