Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 14:23

Marekani yakashifu Cuba kwa kukandamiza watu wake


Waandamani wa Cuba kwenye mji mkuu wa Havana

Ikulu ya Marekani Jumanne imesema kuwa Marekani inaangalia namna ya kuwasaidia watu wa Cuba walioshiriki kwenye maandamano ya kuipinga serikali ikiongeza kuwa serikali ya Cuba inahitaji kuwajibishwa kutokana na kuminya uhuru wa watu wake.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Psaki amewaambia wanahari kwamba Marekani inajaribu kuwatambua maafisa wa Cuba waliohusika kwenye mashambulizi dhidi ya watu waliokuwa wakiandamana kwa amani.

Ameongeza kusema kuwa Marekani inapanga kuongeza upatikanaji wa internet nchini Cuba, kuongeza misaada ya kibinadamu pamoja na kuweka mikakati itakayo rahisisha utumaji wa fedha kutoka kwa watu wa Cuba walioko nje ya nchi bila kuingiliwa na serikali.

Ameongeza kusema kuwa wamebuni kundi litakalo hakikisha kuwa watu wa Cuba wanapokea fedha zao moja kwa moja kutoka kwa jamaa zao kwa kuwa kwa muda mrefu Marekani imekuwa na wasi wasi kwamba serikali ya Cuba imekuwa ikichukua pesa za watu binafsi zinazotumwa nchini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG