Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 14:12

Waafrika 34 wapotelea baharini wakivuka kwenda Ulaya


Wahamiaji wakisafiri kuingia kwenye mji wa Deal ulioko pwani ya kusini mashariki mwa Uingereza. Picha na BEN STANSALL / AFP.
Wahamiaji wakisafiri kuingia kwenye mji wa Deal ulioko pwani ya kusini mashariki mwa Uingereza. Picha na BEN STANSALL / AFP.

Takriban wahamiaji 34 wa Kiafrika wamepotea siku ya Ijumaa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria ikitokea nchini Tunisia kuzama.

Hii ni ajali ya tano ya meli katika muda wa siku mbili, na kuongeza idadi ya watu waliopotea kufikia 67. Wakati huo huo kumekuwa na ongezeko kubwa la boti zinazoelekea nchini Italia, maafisa wa Tunisia walisema.

Walinzi wa pwani wa Italia wamesema Alhamisi lwamewaokoa takriban wahamiaji 750 katika operesheni mbili tofauti kwenye ukanda wa pwani kusini mwa nchi hiyo. Saa kadhaa baadaye watu wengine wasiopungua watano walifariki dunia na wengine 33 hawajulikani walipo baada ya kujaribu kuvuka bahari kutoka Tunisia.

Jaji nchini Tunisia Faouzi Masmoudi aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu saba watu pamoja na watoto wachanga na watoto wengine walikufa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka katika pwani ya mji ya Sfax.

Afisa wa jeshi la ulinzi wa pwani Houssem Jebabli, amesema walinzi wa jpwani walisimamisha boti 56 zilizokuwa katika safari katika muda wa siku mbili kuelekea Italia na kuwazuia zaidi ya wahamiaji 3,000, wengi wao wakiwa wanatoka katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, wahamiaji wasiopungua 12,000 ambao wamefanikiwa kufika nchini Italia mwaka huu, waliingia kwa meli kupitia Tunisia, ikilinganishwa na watu 1,300 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Hapo awali, Libya ilikuwa sehemu kuu ya kivuko iliyokuwa ikitumiwa na wahamiaji kutoka Afrika.

Ukanda wa pwani wa mji wa Sfax umekuwa mashuhuri ukitumiwa na watu wanaokimbia umaskini na migogoro katika nchi za Afrika na Mashariki ya Kati na kujaribu kutafuta maisha bora katika nchi za Ulaya.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG