Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 16:07

Wahamiaji 43 wafariki katika ajali ya boti Italia


Waokoaji wakitafuta manusura baada ya ajali ya boti karibu na ufukwa mjini Crotone, Italia.

Maafisa wa Italia wanasema boti iliyotengenezwa kwa mbao iliyokuwa imewabeba wahamiaji kuelekea Italia ilisambaratika kabla ya kufika ufukweni na kusababisha vifo vya watu 43 akiwemo mtoto mchanga.

Mamlaka zinasema takriban watu 80 walinusurika kwenye mkasa huo. Baadhi ya miili ilioshwa ufukweni Jumapili katika eneo la mapumziko la bahari katika mkoa wa Crotone.

Takriban watu 100 walikuwa ndani ya meli hiyo, maafisa walisema. "Ni janga kubwa," Meya wa Crotone Vincenzo Voce alisema.

Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis alisema Jumapili, "Ninaombea kila mmoja wao, kwa wale wasiojulikana waliko na wahamiaji wengine walionusurika."

Papa Francis pia alisema alikuwa akiombea waokoaji "na wale wanaowakaribisha" wahamiaji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG