Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 23:33

Watu 22 wafariki katika ajali ya mashua Madagascar


Mtu mmoja akisafiri kwa mashua kuvua samaki kwenye dimbwi nje kidogo ya mji mkuu Antananarivo, kwenye picha hii ya tarehe 30 Oktoba 2013.
Mtu mmoja akisafiri kwa mashua kuvua samaki kwenye dimbwi nje kidogo ya mji mkuu Antananarivo, kwenye picha hii ya tarehe 30 Oktoba 2013.

Watu 22 walifariki dunia wakati mashua iliyokuwa imewabeba kutoka Madagascar ilipopinduka walipokuwa wakijaribu kusafiri kuelekea kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte, mamlaka ya bandari ya Madagascar ilisema Jumapili.

Boti hiyo iliyokuwa imebeba watu 47, ilipinduka siku ya Jumamosi katika bahari ya Ankazomborona kaskazini mwa Madagascar, mamlaka ya Bahari na Mito lilisema katika taarifa.

Shirika hilo limesema boti hiyo ilipata ajali, ambapo 23 kati ya waliokuwemo waliokolewa, huku miili 22 ikipatikana. Wengine wawili bado walikuwa hawajulikani waliko.

Afisa wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema wengi wa waliookolewa walikimbia ili kuepuka kukamatwa kwa kujaribu kusafiri hadi Mayotte.

XS
SM
MD
LG