Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:31

Takriban wahamiaji 60 wafariki katika ajali ya boti Italia


Waokoaji wakiokoa mIili baada ya mashua inayoshukiwa kuwa ya wahamiaji kuhpata ajali na miili inayoaminika kuwa ya wakimbizi kupatikana Cutro, pwani ya mashariki ya eneo la Calabria nchini Italia, Februari 26, 2023.REUTERS
Waokoaji wakiokoa mIili baada ya mashua inayoshukiwa kuwa ya wahamiaji kuhpata ajali na miili inayoaminika kuwa ya wakimbizi kupatikana Cutro, pwani ya mashariki ya eneo la Calabria nchini Italia, Februari 26, 2023.REUTERS

Takriban wahamiaji 59, wakiwemo watoto 11 na mtoto mchanga mmoja, walifariki dunia  baada ya boti yao iliyokuwa imejaa  kuzama mapema Jumapili kwenye hali ya  dhoruba ya baharini  karibu na eneo la kusini mwa Italia la Calabria, maafisa walisema.

Kufikia dakika chache zilizopita, idadi ya waathirika waliothibitishwa ilikuwa 59, Vincenzo Voce, Meya wa jiji la pwani la Crotone, alikiambia kituo cha televisheni cha Sky TG-24 Jumapili alasiri.

Kituo cha uokoaji cha Crotone kilisema 12 kati ya waathirika 59 walikuwa ni watoto, pamoja na mtoto mmoja mchanga, na 33 walikuwa wanawake, kwa mujibu wa shirika la habari la AGI.

Walinzi wa pwani wa Italia walisema boti hiyo iliyojaa mizigo ilipasuka katika mawimbi makali karibu na Crotone, huku afisa mmoja akiripoti kuwa mtu anayeshukiwa kuwa mlanguzi wa watu amekamatwa na vikosi vya usalama.

Mabaki ya mbao yalitapakaa karibu mita 100 kwenye ufukwe, ambapo waokoaji wengi walipelekwa, mwandishi wa habari wa AFP alishuhudia.

Wafanyakazi wa uokoaji waliiambia AFP kwamba boti hiyo ilikuwa imebeba zaidi ya watu 200.

XS
SM
MD
LG