Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:16

Virusi vya Corona vinaweza kubakia katika mazingira hadi siku 28 - Utafiti


Wafanyakazi wa afya wakisaidia watu kufanya vipimo vya COVID-19 mjini Picton, Sydney, Australia Julai 15, 2020. (Photo by SAEED KHAN / AFP).
Wafanyakazi wa afya wakisaidia watu kufanya vipimo vya COVID-19 mjini Picton, Sydney, Australia Julai 15, 2020. (Photo by SAEED KHAN / AFP).

Wanasayansi nchini Australia wanasema wamegundua kuwa virusi vya corona vinaweza kubaki hai kwenye mazingira hadi siku 28.

Katika utafiti uliochapishwa mapema Jumatatu kupitia jarida linaloangazia masuala ya virusi la Virology Journal, idara ya utafiti wa kitaifa ya Australia imegundua kwamba virusi vya COVID-19 vinaweza kubaki hai kwenye mazingira wakati viwango vya joto viko katika degree 20 celcius kwa siku.

Utafiti huu umeangaza hili ukilinganisha na vile vya homa ya kawaida ambavyo vinabaki hai kwa siku 17 kwenye mazingira kama hayo.

Watafiti hao pia wamegundua kuwa virusi hivyo vinapoteza uwezo wa kuambukizwa baada ya takriban saa 24 kwenye mazingira ya joto ya degree 40 celcius.

Inasemakana kuwa virusi hivyo vinabaki hai kwenye vifaa kama noti, glasi na vyuma.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson leo Jumatatu anatarajiwa kuzindua mikakati mipya ya kukabiliana na maambukizi ya virui vya corona.

Kupitia hotuba kwenye bunge, kiongozi huyo anatarajiwa kueleza kuhusu hatua za kuchukukiwa kulingana idadi ya maambukizi katika maeneo tofauti ya nchi.

Hatua hizi zinachukuliwa wakati taifa hilo likisemekana linashuhudia ongezeko la maambukizi hasa kwenye miji kaskazini ya Liverpool, Manchester, Newcastle na Mereyside.

Kufikia sasa taifa hilo limeshudia takriban vifo 42, 825 kutokana na virusi vya corona ikiwa mojawapo ya idadi kubwa zaidi barani Ulaya.

XS
SM
MD
LG