Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 12:02

Wamarekani wasema Harris na Pence hawakujibu baadhi ya masuala katika mdahalo


Mwendesha mdahalo Susan Page (kushoto) akionyesha ishara kwa Makamu wa Rais Mike Pence (kulia) wakati yeye na mgombea wa chama cha Demokratik na Seneta kutoka California, Kamala Harris wakishiriki katika mdahalo uliofanyika ukumbi wa Kingsbury, Chuo Kikuu cha Utah Oct 7, 2020.
Mwendesha mdahalo Susan Page (kushoto) akionyesha ishara kwa Makamu wa Rais Mike Pence (kulia) wakati yeye na mgombea wa chama cha Demokratik na Seneta kutoka California, Kamala Harris wakishiriki katika mdahalo uliofanyika ukumbi wa Kingsbury, Chuo Kikuu cha Utah Oct 7, 2020.

Wamarekani wengi wanahisi mdahalo kati ya Makamu wa Rais Mike Pence na mgombea mwenza wa chama cha Demokratik Seneta Kamala Harris haujazungumzia jambo lolote jipya na wagombea hao mara nyingi hawakujibu baadhi ya masuala walioulizwa na mwendesha mdahalo Susan Page.

Hata hivyo mwandishi wa Sauti ya Amerika anaripoti kwamba suala la jinsi utawala wa Rais Donald Trump ulivyokabiliana na janga la COVID-19 lilichukuwa nafasi ya juu, wakati rais na baadhi ya washauri wake wakiwa wanaugua ugonjwa huo.

Kulingana na utafiti wa maoni wa vyombo mbali mbali ni kwamba Wamarekani wamegawika karibu sawa juu ya nani ameweza kutetea vilivyo ajenda yao katika mdahalo wa kwanza na wa pekee kati cha makamu rais uliozungumzia masuala mbali mbali ya ndani, uchumi na kimataifa lakini kugubikwa na habari juu ya kuambukizwa kwa rais Trump na washauri wake wa White House na virusi vya corona.

Akianza tu mdahalo Harris amesema Trump amekabiliana vibaya sana na janga hilo la corona.

Donald Trump
Donald Trump

Harris ameeleza :"Wamarekani wameshuhudia kile ambacho ni kushindwa vibaya sana kufanya kazi kwa utawala ulioko madarakani katika historia ya nchi yetu.

Haikuwa hivyo alijibu Pence akidai Trump alisitisha safari kutoka China, kitovu cha virusi hivyo, akipunguza kasi za kusambaa kwa ugonjwa mwishoni mwa mwezi Januari.

Pence alifafanua hilo akisema : "Kwa mara nyingine tena Wamarekani wanahaki kufahamu kwamba Joe Biden alipinga uamuzi wa Rais Trump Kusitisha safari zote kutoka China.

biden
biden

Zaidi ya hayo Pence na Harris walizungumzia juu ya namna utawala wa Trump ulivyokabiliana na uchumi, sera za kigeni, mabadiliko ya hali ya hewa, ukosefu wa ajira na vita vya biashara na China.

Harris aliongeza kuwa kwa sababu ya hicho kinachojulikana kama vita vya biashara na China, Marekani imepoteza nafasi laki tatu za ajira katika viwanda.

Naye Pence kwa mara nyingine akipinga jambo hilo akisema : " Tumepoteza vita vya biashara na China? Joe Biden hajapata kamwe kupigania vita hivyo. Biden amekua mtetezi wa China ya kikomunisti mnamo miongo kadhaa sasa.

Suala tete kwenye mdahalo lilikuwa pia mvutano kati ya Warepublican na Wademokrat juu ya kuteuliwa kwa jaji mconservative

Judge Amy Coney Barrett, President Donald Trumps nominee for the U.S. Supreme Court, meets with Sen. Cindy Hyde-Smith, R-Miss., on Capitol Hill in Washington, Wednesday, Sept. 30, 2020. (Oliver Contreras/Pool via AP)
Judge Amy Coney Barrett, President Donald Trumps nominee for the U.S. Supreme Court, meets with Sen. Cindy Hyde-Smith, R-Miss., on Capitol Hill in Washington, Wednesday, Sept. 30, 2020. (Oliver Contreras/Pool via AP)


kuchukuwa nafasi katika mahakama ya juu ya hayati jaji Ruth Bader Ginsburg aliyefariki mwezi uliyopita.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kazi kubwa ya wagombea kiti cha makamu wa rais katika mdahalo ni kuepusha kufanya makosa yatakayo umiza misimamo ya wagombea wenza wao.

Kwa upande wake Profesa Anra Gillespie wa Chuo Kikuu cha Emory anasema wagombea hao waliweza kutetea sera zao vizuri.

Gillespie anasema : "Ninadhani kwa sehemu kubwa walifanikiwa kutodhuru kampeni zao. Hivi sasa Makamu wa Rais Pence yuko katika hali tofauti kwa sababu yeye ni sehemu ya serikali inayotetea madaraka yake, na hivyo ni lazima ajibu kasoro na mafakinio ya utawala wa Trump.

Naye Rich Meagher wa Chuo Kikuu cha Randolph-Macon anasema mdahalo huu ulikuwa na umuhimu mkubwa katika uchaguzi huu, ambapo karibu watu milioni 4 wameshapiga kura zao katika majimbo yanayoruhusu upigaji kura mapema.

Meagher anafafanua : Watu hawampigi kura Makamu rais, wanawapigia kura rais. Lakini mwaka 2020 mambo ni tofauti. Tuna wagombea wawili wazee kuliko wakati mwengine wowote ule. Tuna mgombea mmoja anaetetea kiti chake ambaye anaugua ugonjwa mmoja wa hatari.

Na hivyo wagombea hao wa nafasi ya makamu wa rais wanalazimika kuwa tayari kuchukua nafasi ya rais ikiwa rais atafariki akiwa madarakani au hawezi kufanya kazi zake.

Mbali na mdahalo huo wiki hii mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik Joe Biden alikuwa katika jimbo lenye ushindani mkubwa la Florida na kuhudhuria mkutano na wapiga kura ulioandaliwa na kituo cha NBC kueleza sera zake juu ya masuala mbali mbali na namna atakavyo tawala kwa tofauti na utawala wa Rais Trump.

Trump naye alirudi White House Jumatatu baada ya kulazwa hospitali kwa siku tatu kutokana na kuambukizwa na virusi vya corona, ugonjwa ambao umemsababisha kusitisha kampeni zake kwa muda.

Hadi hivi sasa utafiti wa maoni unaonyesha Biden akiongoza kwa wastani asilimia 10 dhidi ya Trump na yuko katika nafasi nzuri kwenye majimbo yenye ushindani mkubwa.

Inaripotiwa kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani idadi kubwa kabisa ya wapiga kura wametumia njia ya posta kupiga kura zao na tayari mamilioni wameshapeleka kura zao.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG