Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:19

Trump atoka hospitalini


Rais wa Marekani Donald Trump punde tu baada ya kutoka kwa hospitali ya Walter Reed mjini Bethesda, Maryland Jumatatu jioni. Oktoba 5, 2020.
Rais wa Marekani Donald Trump punde tu baada ya kutoka kwa hospitali ya Walter Reed mjini Bethesda, Maryland Jumatatu jioni. Oktoba 5, 2020.

Rais wa Marekani Donald Trump alitoka hospitalini Jumatatu jioni saa za Washington baada ya kuwapo kwa takriban saa 72.

Trump alitoka kwenye hospitali ya Walter Reed iliyo mjini Bethesda, jimbo la Maryland mwendo wa saa kumi na mbili na dakika thelathini na tisa na kupelekwa kwa gari hadi kwenye helikopta ya kijeshi iliyokuwa imeegeshwa karibu na hospitali hiyo na kuondoka bila kuwahutubia waandishi wa habari.

Mapema Jumatatu, daktari wa rais huyo, Sean Conley, alisema kwamba ingawa hakuwa amepona kabisa, vipimo walivyovifanya vilionyesha kwamba ni sawa kwake kurejea kwenye ikulu.

"Ndani ya White House kuna wataalam wa afya wanaoweza kumwangalia saa 24 kwa siku," alisema Dkt Conley.

Kila siku mgonjwa anapoendelea kukaa kwa hospitali bila haja ya kuwa mle, anahatarisha maisha yake. Kwa sasa hakuna husduma yoyote anayopata hapa hospitalini anmabayo hawezi kupata kwa ikulu," aliongeza.

Kwa mujibu wa madaktari, Trump anendelea kutibiwa kwa dawa aina tatu ikiwemo ile ya Remdesivir, ambayo iko kwa awamu ya majaribio.

Iliripotiwa Ijumaa wiki iliyopita kwamba Trump na mkewe Melania Trump, walikuwa wameambukizwa virusi vya corona, na baadaye siku hiyo, Rais huyo akapelekwa hospitalini.

Tangu wakati huo, maafisa kadhaa waandamizi katika utawala wa Trump pamoja na wanasiasa wameripotiwa kuambukizwa virusi hivyo. Wa hivi karibuni kabisa ni msemaji wa ikulu Kayleigh McEnany, aliyeandika kwenye ukurasa wake Jumatatu asubuhi kwamba ameambukizwa.

Trump amekuwa miongoni mwa viongozi wa dunia walioambukizwa ugonjwa huo, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Rais wa Honduras Juan Orlando Hernandez, Rais wa Bolivia Jeanine Anez na kiongozi wa Armenia Nikol Pashinyan.

XS
SM
MD
LG