Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 11:49

Kuugua Trump COVID-19 kwazusha mjadala juu ya uchaguzi wa rais Novemba


Wafuasi wa Rais Donald Trump wakiwa nje ya Hospitali ya Kitaifa ya Walter Reed Bathesda, Maryland Octoba 4, 2020.

Macho na masikio ya Wamarekani na takriban dunia nzima wiki hii yanaelekezwa katika afya ya Rais Donald Trump ambaye amelazwa hospitali tangu Ijumaa akiugua ugonjwa wa COVID-19.

Trump pamoja na mkewe Melania na washuari wake wa karibu wameambukizwa virusi vya corona na kuzusha suala juu ya hali hiyo itakavyo badili kinyang'anyiro cha ya uchaguzi wa urais 2020 ikiwa imebaki chini ya mwezi moja kufanyika.

Rais Donald Trump na mkewe Melania
Rais Donald Trump na mkewe Melania

Kumekuwepo na habari za kutatanisha mwishoni mwa wiki juu ya hali ya Rais Trump, kutoka kwa madaktari wake na washauri wake na mambo mengi hayafahamiki Ikiwa ni pamoja na jinsi kampeni zitakavyo endelea kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Novemba 3.

Kufuatana na takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins, zaidi ya watu milioni 35 kote duniani wameambukizwa na virusi hivyo.

Na kutokana na hayo katika video aliotoa Jumamosi akiwa hospitali, Trump amesema amepata funzo kutokana na hali yake ya kupambana na virusi hivyo na sasa itakuwa ni kazi yake kuwasaidia wengine.

Donald Trump : "Lakini hii ni kitu kinachotokea. Na kimewakumba mamilioni ya watu kote duniani. Ninapambana kwa ajili yao. Ninapambana kwa wote walioathirika duniani. Tutavishinda virusi hivi vya corona, na tutavishinda kwa nguvu."

Hapo Jumapili madaktari wa rais walisema wanamtibu na aina tatu za dawa na wanataraji atarudi White House baadae Jumatatu. Jambo ambalo waatalamu wengi wa afya wamehoji ikiwa itakuwa hatua ya busara.

Kamanda wa Jeshi la Majini Dkt Sean Conley, daktari wa Rais, akiwa na madaktari wengine akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya Rais.
Kamanda wa Jeshi la Majini Dkt Sean Conley, daktari wa Rais, akiwa na madaktari wengine akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya Rais.

Hata hivyo, habari kwamba Trump anapata nafuu zimesababisha bei za hisa za Ulaya na Asia kupanda Jumatatu hadi kufikia asilimia 2 na bei za mafuta ghafi pia zimepanda kufikia asili mia 2.

Mchambuzi wa masoko mjini Frankfurt Oliver Roth akizungumza na shirika la Habari la Reuters anasema kwa vile wawekezaji wanampendelea Trump zaidi kuliko mpinzani wake, Biden masoko lazima yaimarike kutoka hali ya waswasi wiki iliyopita.

Roth Mchambuzi wa masoko ya hisa katika Benki ya Oddo Seydler anasıma : "Masoko ya Hisa na wawekezaji wanampendelea zaidi Trump kwa vile anatetea kuondosha masharti ya biashara, kupunguza kasi na kupatikana fedha kwa urahisi. Kwa hivyo alipopimwa na COVID-19 kulikuwa na hali ya wasiwasi katika masoko."

Ugonjwa wa rais umetokea wakati yeye na mpinzani wake makamu rais wa zamani Joe Biden wanaingia katika awamu ya mwisho ya wiki nne za kampeni kabla ya siku ya uchaguzi mkuu.

Kampeni za Trump zimesitishwa kwa muda wakati Biden anaendelea na kampeni, na mdahalo kati ya makamu rais Mike Pence na mgombea mwenza wa Biden Kamala Harris utaendelea kama ulivyopangwa siku ya Jumatano.

Maafisa wa Kampeni ya Trump hadi sasa hawajasema lolote juu ya namna wataendelea na mipango yao katika wakati huu muhimu, isipokuwa mshauri muandamizi Jason Miller anamtetea Trump akisema amekuwa akichukuwa tahadhari za kutosha na amedhihirisha kuwa ni kiongozi katika vita dhidi ya virusi hivi.

Jason Miller anaeleza : "Vile vile kama tulivyoshuhudia alichofanya Joe Biden. Nikimaanisha hatuwezi tu kujifungia ndani maisha yetu yote. Inatubidi tutoke nje na kuishi maisha yetu na kukabiliana na hali hii, kutengeneza chanjo na tiba zaidi ili kuweza kuushinda uogonjwa huu."

Matokeo ya utafiti kadhaa ya maoni ya wapiga kura yanaonyesha Biden yungali anaongoza. Jambo moja linalofahamika wazi ni kwamba hakuna anayejua kile kitakachoweza kutokea katika muda uliobaki katika kinyan’ganyiro kilichokuwa na ushindani mkubwa kugombania kiti cha White House.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG