Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 01, 2023 Local time: 16:08

Taarifa za ulipaji kodi wa rais Donald Trump zatoka


Rais wa Marekani, Donald Trump, akiongea na wanahabari White House, Septemba 27, 2020.

Gazeti la New York Times,Jumapili limeripoti kwamba rais wa Marekani, Donald Trump alilipa kodi ya dola 750 pekee mwaka aliowania urais.

Kiwango hicho alicholipa kodi ni kutoka katika mapato yake mwaka 2016, na mwaka wa kwanza alipoanza kuhudumu kama rais wa Marekani.

Gazeti la New York Times linasema rais Trump ni rais pekee katika ulimwengu wa sasa ambae hakulipa kodi katika kipindi cha miaka 10 katika miaka 15 iliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumapili, akiwa White House, rais Trump ametupilia mbali ripoti hiyo ya New York Times, kwa kusema ni uzishi.

Vilevile amesema kwamba licha ya huo kuwa ni uzishi, amekuwa akilipa kodi ingawaje lakini kutoa maelezo zaidi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG