Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 14:55

Rais Trump asema anaendelea vizuri


Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye ameambukizwa virusi vya Corona.
Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye ameambukizwa virusi vya Corona.

Zaidi ya wiki moja baada ya kuambukizwa virusi vya corona, rais wa Marekani, Donald Trump, Jumapili, amesema anajisikia yuko vizuri sana, na hatumii dawa yoyote.

Katika mahojiano kwa njia ya simu na televijeni ya Fox news, Trump, amesema, "nimevishinda virusi hivi vibaya vya China, ni kama nina kinga ya mwili labda kwa muda mrefu, muda mfupi, labda maisha yangu yote.”

Lakini katika mahojiano hayo, mwanahabari hakumuuliza iwapo vipimo vilionyesha kwamba hana tena virusi vya corona, ambavyo vimesha ua zaidi ya watu laki mbili, na kuambukiza zaidi ya millioni saba ncini Marekani.

Muda mfupi baada ya kufanya mahojiano na televijeni ya Fox, Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, kwamba madaktari wake wamethibitisha kuwa amepona kabisa, na kuongeza kuwa hivi sasa hawezi kuambukizwa Corona, wala hawezi kuwaambukiza watu wengine.

Baadae kampuni ya Twitter imesema “ujumbe wa Trump unakiuka maadili ya mtandao wa Twitter kuhusu kusambaza habari za uongo, na kupotosha za janga la Covid-19.

XS
SM
MD
LG