Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 20:03

Vikosi vya pamoja Afrika Magharibi vya ripoti waasi zaidi ya 100 wameuawawa


Magari yaliyochomwa moto na washukiwa wanachama wa by Islamic State, Jimbo la Afrika Magharibi (ISWAP) walipofanya shambulizi February 9, 2020 na kuwateka Watu wasiopungua 30 na wanawake na watoto kutekwa Jimbo la Borno, msemaji wa serikali alisema February 10, 2020. (AFP)

Vikosi vya pamoja vya kijeshi kutoka Nigeria, Niger na Cameroon vimesema Jumapili kuwa vimewauwa zaidi ya wanamgambo 100 waasi wa Kiislamu wenye msimamo mkali.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kati ya waliouwawa ni makamanda 10 wa wanamgambo hao katika wiki chache zilizopita wakati vikosi hivyo vikiongeza mashambulizi ya ardhini na anga katika eneo la Ziwa Chad.

Wapiganaji wa Boko Haram na kundi lililojitenga la Islamic State katika jimbo la Afrika Magharibi ( ISWAP) kwa zaidi ya muongo mmoja wamekuwa wakipambana na jeshi la Nigeria katika mzozo ambao umekithiri kwenye mataifa jirani.

Msemaji wa kikosi kazi cha pamoja cha kimataifa Kanali Muhammad Dole alisema kuwa wanajeshi wameingia ndani katika mapango yanayodhibitiwa na waasi kwenye eneo la Ziwa Chad na kukamata silaha kadhaa , vyakula na dawa haramu.

Dole hakueleza kipindi cha operesheni au idadi ya wanajeshi waliouwawa lakini amesema wanajeshi 18 walijeruhiwa na mabomu ya kutengenezwa yaliyowekwa na waasi waliokuwa wakiondoka.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG