Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:46

Raia takribani 300 wameuawa nchini Mali; HRW inasema


Wanajeshi wa mali wakiwa katika doria barabarani
Wanajeshi wa mali wakiwa katika doria barabarani

Wanajeshi wa Mali na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Russia waliwauwa takribani raia 300 mwishoni mwa mwezi Machi kati-kati mwa taifa lililokumbwa na mzozo la Sahel, Human Rights Watch (HRW) ilisema Jumanne.

Katika ripoti hiyo kundi la haki za binadamu lilidai mauaji hayo yanayodaiwa kufanywa kwa muda wa siku nne katika mji wa Moura ulioko kati-kati mwa Mali yalikuwa uhalifu wa vita.

Wanajeshi wa Mali na wapiganaji wa kigeni wazungu waliwasili katika mji huo kwa helikopta hapo Machi 27 na kurushiana risasi na kiasi cha wapiganaji 30 wa kiislam, mashahidi kadhaa waliiambia Human Rights Watch. Baadhi ya wanajihadi walijaribu kujichanganya na wakaazi wa eneo hilo.

Katika siku zilizofuata wapiganaji wa Mali na wa kigeni walishutumiwa kuwafunga kamba watu na kuwaua katika vikundi vidogo. HRW ilikadiria kuwa takribani watu 300 waliuawa huku idadi kubwa ya waathirika ni kutoka kabila la Fulani.

XS
SM
MD
LG