Chanzo kimesema “ Shambulio la kigaidi la Jumatano alasiri ambalo lilifanywa na watu wenye silaha nzito waliokuwa kwenye pikipiki na ndani ya gari liliua watu 19 waliokuwa wanasafiri kwa basi, mkiwemo afisa wawili wa polisi”.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa watu wengine wawili waliuawa katika shambulio dhidi ya lori ambalo lilichomwa moto na washambuliaji.
Watu watano akiwemo afisa moja wa polisi walijeruhiwa katika shambulio dhidi ya basi ambalo nalo lilichomwa moto.