Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:14

Askari polisi 13 wauawa na watu wenye silaha nchini Burkina Faso


Wanajeshi wa Burkina Faso wakipiga doria karibu na kituo cha jeshi la ulinzi wa rais mjini Ouagadougou, Septemba 29, 2015. Picha ya AFP.
Wanajeshi wa Burkina Faso wakipiga doria karibu na kituo cha jeshi la ulinzi wa rais mjini Ouagadougou, Septemba 29, 2015. Picha ya AFP.

Watu wenye silaha waliua askari polisi 13 Jumapili katika shambulio la kuvizia katika mji wa madini wa Burkina Faso wa Taparko

Chanzo cha usalama kimeiambia AFP kwamba “Kikosi cha askari polisi kimejikuta katika shambulio la kuvizia la watu wenye silaha Jumapili mchana karibu na mji wa Taparko. Watu 13 walithibitishwa kuuawa, na kuna askari polisi wengine waliotoweka”, chanzo hicho kimeongeza.

Askari polisi wengine 8 walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Taparko ni mji wa madini ambao umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wapiganaji wanajihadi.

Taarifa kuhusu shambulio hilo zimetolewa wakati watu 2 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya basi lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini Jumapili, karibu na mji wa Taparko.

Jumapili pia, watu 11 waliuawa katika shambulio kwenye mgodi wa dhahabu katika mji wa kaskazini wa Baliata.

XS
SM
MD
LG