Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:48

Jeshi la Mali linasema limeua wanamgambo wa kiislamu 19


Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, Kanali Assimi Goita akizungumza na waandishi wa habari, Septemba 22, 2020. Picha ya AFP
Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, Kanali Assimi Goita akizungumza na waandishi wa habari, Septemba 22, 2020. Picha ya AFP

Jeshi la Mali limesema limewaua wapiganaji wa kiislamu 19 katika operesheni kaskazini mashariki mwa mji mkuu Bamako, ambazo ziliungwa mkono na wanajeshi maalum wa Umoja wa Ulaya.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa jeshi la Mali Jumanne jioni ilisema operesheni katika wilaya za Timbuktu, Segou, Mopti na Bandiagara ziliwalenga kwa maafanikio magaidi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa ngome zao 15 zilivunjwa, pikipiki 34 zilikamatwa na 15 ziliharibiwa, na simu za mkononi 37 zilichukuliwa, taarifa hiyo imesema.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu 18 walikamatwa katika eneo la Timbuktu.

Wanajeshi wa Mali walishirikiana na wanajeshi maalum wa Umoja wa Ulaya katika operesheni iliyopewa jina la “ Takuba”, taarifa ya jeshi imesema.

Kushirikiana huko kwa jeshi la Mali na kikosi maalum cha Umoja wa Ulaya ni baada ya malumbano kati ya Ufaransa na utawala wa kijeshi wa Mali.

Malumbano hayo yalipelekea rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kutangaza Alhamisi iliyopita kwamba wanajeshi wa Ufaransa ambao walikuwa wakipambana na wanajihadi kwa kipindi cha miaka tisa, wataondoka nchini Mali.

XS
SM
MD
LG