Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:22

UN yaripoti watu zaidi ya 84,000 walazimika kukimbia makazi yao Sudan


Raia wa Darfur waliopoteza makazi yao.
Raia wa Darfur waliopoteza makazi yao.

Umoja wa Mataifa umeripoti Alhamisi kwamba ghasia magharibi mwa Sudan mwezi huu pekee  zimewakosesha makazi watu zaidi ya 84,000.

Umoja wa mataifa umeripoti Alhamisi kwamba ghasia magharibi mwa Sudan mwezi huu pekee zimewakosesha makazi watu zaidi ya 84,000.

Imeongeza kuwa idadi hiyo ikiongezeka mara mbili ya wale ambao wameondolewa katika nyumba zao hadi sasa mwaka 2022.

Idadi hiyo ni kubwa kuanzia mwezi Januari mwaka 2021. Mwaka jana takriban watu zaidi ya laki nne walikoseshwa makazi , mara tano zaidi ya mwaka 2020 hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.

Mzozo umezuka huko baada ya mwaka 2003 baada ya serikali ya Sudan kujiunga na kundi la wanamgambo la Janjaweed kwa ajili ya kupambana na makundi ya uasi yenye silaha.

Takriban watu milioni 2.5 walikoseshwa makazi na wengine 300,000 waliuwawa.

XS
SM
MD
LG