Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:45

Watu 168 wauawa katika mapigano ya kikabila nchini Sudan


Ramani ya Sudan inaonyesha maeneo ya Kaskazini, Kusini na Darfur magharibi.
Ramani ya Sudan inaonyesha maeneo ya Kaskazini, Kusini na Darfur magharibi.

Mapigano kati ya makundi hasimu katika jimbo la Sudan la Darfur yamesababisha vifo vya watu 168 Jumapili, kundi moja la misaada limesema.

Ghasia zilizuka kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa na bado zinaendelea katika eneo la Krink la Darfur magharibi, amesema Adam Regal, msemaji wa shirika la uratibu wa wakimbizi na waliokoseshwa makazi yao katika jimbo la Darfur, likiwa kundi huru la misaada.

Kundi hilo limesema watu 8 waliuawa Ijumaa pekee.

Regal amesema watu 46 walijeruhiwa katika mapigano, na kuelezea wasiwasi wake kwamba idadi ya waliouawa inaweza kuongezeka.

Kiongozi wa kabila la wachache wasiokuwa Waarabu la Massalit ameelezea kuona maiti nyingi katika vijiji vya eneo la Krink, ambalo liko umbali wa kilomita 80 kutoka mji mkuu wa jimbo la Darfur, Geneina.

Jumapili, shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limetoa wito kwa viongozi kuhakikisha majeruhi wanafikishwa salama kwenye hospitali.

Ghasia za hivi karibuni zilizuka baada ya watu wenye silaha wa kabila la Waarabu kushambulia vijiji vya walio wachache wa kabila la Massalit kulipiza kisasi mauaji ya Alhamisi ya watu wawili kutoka kabila lao, kundi hilo la misaada limesema.

XS
SM
MD
LG