Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 04:09

UN yakadiria vifo kutokana na vita Yemen kufikia 377,000 mwisho wa 2021


Watu wakiwa katika pikipiki wakipita katika eneo ambalo shambulizi la angani lilifanywa na Ushirika wa nchi zinazoongozwa na Saudi Arabia huko Sanaa, Yemen November 11, 2021. REUTERS/Khaled Abdullah

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inakadiria idadi ya vifo kutokana na vita vya Yemen itafikia 377,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2021.

Idadi hii itajumuisha wale waliouawa kutokana na sababu zisizo za moja kwa moja na za moja kwa moja.

Katika ripoti iliyochapishwa Jumanne na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa - UNDP, linakadiria asilimia 70 ya wale waliouawa watakuwa ni watoto walioko chini ya umri wa miaka mitano.

Pia imegundua kwamba asilimia 60 ya vifo vinatokana na sababu zilizo za moja kwa moja kama vile njaa, na magonjwa yanayoweza kuzuilika, wakati waliokufa kwa sababu za moja kwa moja zinatokana na kuwa mstari wa mbele katika uwanja wa mapambano, na mashambulizi ya anga.

Yemen imetumbukia katika vita tangu mwaka 2014 wakati waasi wa Kihouthi walipochukua eneo kubwa la upande wa kaskazini mwa nchi ikiwemo mji mkuu wa Sanaa wakati serikali ilipokimbia.

Machi mwaka 2015 ushirika wa nchi za Kiarabu ukiongozwa na Saudi Arabia uliingilia kati vita kwa lengo la kuirejesha serikali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG