Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:27

Waasi wa Houthi Yemen wakaribia kuchuka mji wa Marib


Waasi wa Houthi wa Yemen.
Waasi wa Houthi wa Yemen.

Waasi wa ki Houthi wa Yemen huenda wakabadili hali ya mapigano nchini humo wakati wakisemekana kukaribia kupata udhibiti wa mji muhimu uliopo kaskazini, huku wataalamu wakionya kwamba hali hiyo itaacha mamilioni ya wakimbizi hatarini. 

Mamia ya wapiganaji wameuwawa kwenye mapigano makali mwezi huu baada ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran kuanza upya mashambulizi kwenye mji wa Marib wenye utajiri mkubwa wa mafuta, na ambao ni ngome ya mwisho inayoshikiliwa na serikali kaskazini mwa Yemen.


Iwapo waasi hao watauteka mji huo muhimu, basi sauti yao kwenye meza ya mazungumzo itaongezeka kwa kuwa serikali haitakuwa na udhibiti wowote upande wa kaskazini.Hali hiyo pia inazua wasi wasi kuhusu zaidi ya wakimbizi milioni 2 wanaoishi kwenye makambi baada ya kutoroka kutoka maeno mengine ya nchi.

Tishio la Marib limekuja miaka 7 baada ya waasi kuchukua mji mkuu wa Sanna uliyoko kilomita 120 mashariki ma Marib.

XS
SM
MD
LG