Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 05:57

UN : Mashambulizi ya angani yauwa zaidi ya raia 30 Yemen


Baada ya shambulizi la angani watu wakipekuwa kifusi kutafuta miili katika jimbo la Al-Jawf , Yemen, Februari 15, 2020. Houthi Media Centre/via REUTERS.

Mashambulizi ya angani yameuwa zaidi ya raia 30 katika eneo la milimani kaskazini mwa jimbo la Yemen Jumamosi, mkuu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, UN, nchini humo amesema, na kusema shambulizi hilo ni la kutisha.

Waasi wa Yemen, wanaojulikana kama Wahouthi, wameushutumu ushirika wa majeshi yanayo ongozwa na Saudi kwa kufanya mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi baada ya wao kutungua ndege ya kivita ya ushirika huo katika jimbo la Jawf.

Shirika la habari la serikali ya Saudi Arabia limemkariri Kanali Turki al-Maliki, msemaji wa ushirika huo, akisema inafanya uchunguzi “juu ya hasara inayoweza kuwepo” kufuatia operesheni ya uokoaji katika eneo hilo baada ya ndege ya kivita aina ya Tornado kutunguliwa jioni Ijumaa.

Al-Maliki amekaririwa akisema ndege hiyo ilikuwa inatoa msaada wa angani kwa majeshi ya serikali ya Yemen yanayopigana na Wahouthi.

Amesema marubani wawili wa ndege hiyo aina ya Tornado walifanikiwa kuchomoka kwa salama kabla ya ndege hiyo kuanguka, wakidai kuwa Wahouthi waliwashambulia kwa bunduki. Amesema Wahouthi wanajukumu juu ya uhai na usalama wa marubani hao,” kwa mujibu shirika la habari la Saudi Arabia.

Hakusema iwapo kulikuwa na vifo au kutoa maelezo zaidi.

Idadi ya vifo vya raia 'inayoogopesha'

Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa UN nchini Yemen, Lise Grande, amesema “mashambulizi haya ya kinyama” katika wilaya ya Maslub yameuwa raia 31 na kujeruhi 12, kufuatia ripoti ya awali kutoka katika eneo la shambulizi hilo.

“Inatia huzuni.”“Watu wengi wanauwawa Yemen – ni janga kubwa na hakuna uhalali wowote hilo kutokea. Miaka mitano ya mgogoro huu na pande hasimu bado wanashindwa kuwajibika,”amesema Grande

Amesema wengi kati ya wale waliojeruhiwa walipelekwa katika mahospitali huko Jawf na mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Youssef al-Hadri, msemaji wa wizara ya afya inayoendeshwa na Wahouthi, amesema mashambulizi hayo yameuwa watu wasiopungua 32 wakiwemo watoto na wanawake.

Waasi wanaosaidiwa na Iran walitoa picha za kutisha zikionyesha jengo lililokuwa limeharibiwa kabisa na magari na miili ya waliouawa kueleza shambulio hilo.

Pia walionyesha picha za video zikionyesha kuangushwa kwa ndege hiyo ya Saudi Arabia na mabaki ya ndege hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG