Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:50

Ukraine: Majeshi ya Russia yaingia katika viunga vya mji wa Sievierodonetsk


Mtu akihuzunika wakati wa mazishi ya wanajeshi wawili wa Ukraine waliouwawa katika uvamizi wa Russia huko Uzhhorod, mkoa wa Zakarpattia, May 30, 2022.
Mtu akihuzunika wakati wa mazishi ya wanajeshi wawili wa Ukraine waliouwawa katika uvamizi wa Russia huko Uzhhorod, mkoa wa Zakarpattia, May 30, 2022.

Wanajeshi wa Russia wameingia katika viunga vya mji wa  Ukraine wa Sievierodonetsk, Gavana wa mji huo  amesema Jumatatu, akifafanua mapigano makali kutokea na kuuharibu mji na mji huo umekuwa  lengo kubwa la Moscow.

Russia imeelekeza nguvu zake kwenye kituo kikuu cha mwisho cha idadi ya watu ambacho bado kinashikiliwa na vikosi vya Ukraine katika mkoa wa mashariki wa Luhansk, katika harakati za kufikia moja ya malengo yaliyotajwa ya Rais Vladmir Putin baada ya miezi mitatu ya vita.

Mashambulizi ya mara kwa mara ya makombora yamewaacha wanajeshi wa Ukraine wakilinda magofu huko Sievierodonetsk, lakini kukataa kwao kuondoka kumepunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya mashambulizi makubwa ya Russia katika mkoa wa Donbas.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walitakiwa kukutana leo na kesho kujadili kuhusu vikwazo vipya dhidi ya Russia ikiwemo marufuku ya mafuta.

Kabla ya mkutano, waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck alieleza wasiwasi wake kuhusu umoja wa EU kuanza kusambaratika, rasimu ya yaliyojadiliwa iliyoonekana na ROITA imeashiria kwamba kutakuwa na matokeo madogo katika suala la maamuzi mapya.

XS
SM
MD
LG