Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:11

Maafisa wa Ukraine wasema, makombora ya Russia yameua raia 7 katika mji wa Kharkiv


Wazima moto wazima moto kwenye kibanda cha kahawa kilichoangukiwa na kombora mjini Kharkiv, Picha ya AFP
Wazima moto wazima moto kwenye kibanda cha kahawa kilichoangukiwa na kombora mjini Kharkiv, Picha ya AFP

Maafisa katika mji wa pili kwa ukubwa wa Ukraine, Kharkiv, Alhamisi wamesema mashambulizi ya makombora ya Russia yameua raia 7 na kujeruhi wengine 17, huku mapigano makali yakipamba moto kaskazini na mashariki mwa mji huo.

Mashahidi huko Kharkiv wameripoti pia kusikia milipuko ya mara kwa mara wakati wanajeshi wa Russia wakijaribu kuimarisha ngome zao kaskazini mwa mji huo.

Maafisa wa Russia walikuwa bado kutoa maelezo kuhusu matukio hayo karibu na Kharkiv, licha ya mtandao wa kijamii wa jeshi la Russia kujigamba juu ya ushindi wanaoendelea kupata dhidi ya vikosi vya Ukraine, ikiwemo katika eneo la Donbas.

Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani amesema Alhamisi kwamba licha ya ripoti za mapigano yanayoongezeka karibu na Kharkiv, hakuna mabadiliko makubwa kwenye uwanja wa mapambano.

“Bado tunatathmini kuwa vikosi vya Ukraine vimeendelea kuvirudisha nyuma vikosi vya Russia mbali na mji wa Kharkiv,” afisa huyo amesema, akiwataarifu waandishi wa habari kwa masharti ya kutotajwa jina.

XS
SM
MD
LG