Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 03:14

ADB yakusudia kupeleka msaada wa dharura wa mbolea Afrika Magharibi


FILE - Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo ya Afrika, Abidjan, Ivory Coast, Sept. 16, 2016.
FILE - Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo ya Afrika, Abidjan, Ivory Coast, Sept. 16, 2016.

Hatua hiyo ni sehemu ya benki kutangaza dola bilioni 1.5 kusaidi katika uzalishaji wa chakula kwenye bara la Afrika kutokana na athari za uvamizi wa Russia nchini Ukraine, kusaidia katika utoaji wa mbolea wakati bei zinazidi kupanda, ambapo inahatarisha upungufu katika mavuno.

Benki imesema kuna upungufu wa tani milioni mbili za mbolea kote katika bara hilo. imeongeza kusema kuwa imekuwa ikikutana na wakurugenzi wakuu wa makampuni makuu ya mbolea Afrika na wananchi za nje ili kujadiliana jinsi ya kuwa na uwezo wa kupata mbolea bila kuthibitisha kiwango kinachohitajika.

Katika taarifa yake kwenye shirika la habari la ROITA benki ya maendeleo ya Afrika imesema wanazungumza na washirika na wakulima. Kuna uhitaji mkubwa wa mbolea kwa mara mbili, nusu kwa mwezi huu wa Mei na Juni kwa ajili ya kipindi cha baadhi ya upandaji wa mazao, kulingana na maeneo katika bara zima.

Nusu ya pili ni kunyunyuzia mbolea itahitajika katika kipindi kingine cha ukuzaji mazao kinachohitajika baadae, lakini kila nchi itahitaji kuomba kushiriki.

XS
SM
MD
LG