Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:24

Ushawishi wa Russia Afrika wasababisha wasiwasi


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Mawaziri wa ulinzi wa uhispania na Uingereza, wamesema kwamba ushawishi wa Russia unaoendelea Afrika, unatoa tisho kubwa na la kutisha kwa usalama wa mataifa yaliyo katika muungano wa NATO, pamoja na uvamizi wake dhidi ya Ukraine, ni lazima ushughulikiwe na muungano huo wa kijeshi.

Katika kikao na waandishi wa habari mjini Madrid, waziri wa ulinzi wa uhispania Margarita Robles, amesema kwamba kuongezeka kwa oparesheni za serikali ya Russia, pamoja na kundi la mamluki la Wagner, katika nchi kama Mali na Libya, ni ushahidi tosha, akiwalaumu kwa kile amekitaja kama uhalifu wa kupangwa na ugaidi.

Amesema kwamba muungano wa NATO hauwezi kusalia kimya katika swala hilo.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace, amesema kwamba hali ya ukosefu wa usalama inayoendelea kuongezeka, pamoja na ukosefu wa chakula Afrika, huenda ikaathiri Ulaya kwa kiwango kikubwa.

XS
SM
MD
LG