Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 04:21

Zelensky asema yuko tayari kuzungumza moja kwa moja na Putin


Rais Volodymyr Zelensky akikutana mjini Kyiv na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, na waziri wa ulinzi wa Marekani Llyod Austin, April 24, 2022.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Jumatano amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na Russia lakini yatakuwa mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Vladimir Putin.

Akizungumza kwenye mkutano wa uchumi wa dunia kwa njia ya video, Zelensky amesema kuna fursa kubwa ya kumaliza mzozo kati ya Russia na Ukraine ikiwa Putin anaelewa ukweli wa mambo.

Zelensky ameongeza kuwa hatua ya kwanza ili mazungumzo na Russia yafanyike, ni wanajeshi wa Russia kuondoka kwenye mipaka iliyokuwepo kabla ya Russia kuanzisha uvamizi wake mwishoni mwa mwezi Februari.

Huko Russia, Rais Vladimir Putin ametoa amri ambayo itaharakisha mchakato wa kuwapa uraia watu wanaoishi katika maeneo ya Kherson na Zaporizhzhia.

Maafisa wa Ukraine wamesema mapigano ya hivi karibuni kati ya vikosi vya Russia na Ukraine yalifika karibu na mji wa viwanda wa Severodonetsk, wakati wanajeshi wa Moscow wakijaribu kuchukua udhibiti wa eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine baada ya kushindwa kumuondoa madarakani Zelensky na kuuteka mji mkuu, Kyiv.

XS
SM
MD
LG