Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 09:35

Ujerumani na washirika wake waadhimisha miaka 30 tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin


Watu wakiweka maua kwenye mianya ya mabaki ya ukuta wa Berlin katika sherehe za kuadhimisha kuanguka wa utawala wa kikomunisti huko kitongoji cha Bernauer Strasse, Berlin, Ujerumani, Nov. 9, 2019.

Ujerumani imeadhimisha miaka 30 Jumamosi tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin, kipindi muhimu katika historia ambacho utawala wa Kikomunisti Ulaya Mashariki ulimalizika.

Viongozi wa Ujerumani, Poland, Hungary, Slovakia na Jamhuri ya Czech walihudhuria sherehe hizo zilizofanyika Bernauer Strasse --- ambako sehemu ya mabaki ya Ukuta wa Berlin bado yapo --- kabla ya kuweka maua katika mianya ya ukuta huo ambao ulikuwa ni kitisho kwa wanadamu kilichogawanya mji huo kwa miaka 28.

Axel Klausmeier, mkuu wa kituo cha kumbukumbu ya Ukuta wa Berlin, ametaja anakumbuka namna sura za wakazi wa Berlin kutoka Mashariki na Magharibi wakilia kwa furaha wakati walipoweza kufikia familia zao na kwa mara ya kwanza kukumbatiana jioni ya Novemba 9, 1989.

Klausmeier aliwaenzi wale wote walioshiriki katika maandamano ya amani upande Ujerumani Mashariki na nchi za Warsaw waliojitokeza mitaani wakidai uhuru na demokrasia, na ilikuwa ni wakati wa utawala wa Mikhail Gorbachev katika iliyokuwa Umoja wa Soveit aliyeleta mabadiliko makubwa ya sera za kikomunisti.

Maandamano hayo na wimbi la watu waliokuwa wakikimbia kutoka Ujerumani Mashariki iliongeza msukumo wa serikali ya kikomunisti ya nchi hiyo kufungua mipaka yake kwa nchi za Magharibi na hatimaye kumaliza mgawanyiko baada ya taifa hilo kutoka vitani.

Miaka 30 baadae, Ujerumani imekuwa ni uchumi wenye nguvu zaidi na yenye kutegemewa kisiasa katika bara hilo la Ulaya, lakini bado kuna kero nzito kati ya baadhi ya watu katika nchi hiyo, jinsi kipindi cha mpito kilivyoendeshwa katika mabadiliko kutoka uchumi wa ujima kwenda uchumi huru.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kumbukumbu ya tukio hilo kwenye kanisa dogo karibu na sehemu ulipokuwa ukuta kabla ya kuvunjwa, Chansela Angela Merkel aliwaenzi wale wote waliopoteza maisha au kufungwa jela wakijaribu kukimbia kutoka Mashariki kwenda Ujerumani Magharibi na kusisitiza kuwa mapambano ya uhuru duniani hayajamalizika.

"Ukuta wa Berlin, mabibi na mabwana, ni historia na unatufundisha : hakuna ukuta utakao wazuia watu na kuzuia uhuru wao ni mrefu sana au mpana sana kwamba hautaweza kuangushwa," amesema kiongozi huyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG