Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 11:29

Uganda yanyimwa euro milioni 100 ilizoahidiwa na Ujerumani


Wakimbizi kutoka Congo wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali, Uganda, March 19, 2018.
Wakimbizi kutoka Congo wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali, Uganda, March 19, 2018.

Serikali ya Ujerumani haitaipa Uganda euro milioni 100 ilizoiahidi kwa ajili ya makazi ya wakimbizi.

Kwa mujibu wa idhaa ya Kiswahili ya Radio Ujerumani uchunguzi wa Umoja wa Mataifa wa mpango wa ufadhili wa wakimbizi wa Uganda mnamo mwaka 2018 uligundua kuwepo "ufisadi".

Kashfa hiyo ilijitokeza baada ya mvujishaji siri wa ndani ya serikali ya Uganda kuwapasha habari wafadhili kuwa kiasi kikubwa cha fedha kilitolewa kwenye akaunti hiyo.

Uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa, Ofisi ya Ulaya ya Kupambana na Rushwa (OLAF) na serikali ya Uganda uligundua kuwa idadi ya wakimbizi Uganda ilizidishwa kinyume na idadi sahihi ya wakimbizi waliokuwa wako nchini.

Uganda ilisema iliwapa hifadhi wakimbizi milioni 1.3 na kupokea dola milioni 350 kutoka kwa wafadhili mbalimbali mwaka wa 2017. Kwa sasa, Ujerumani itatoa baadhi ya fedha kwa mashirika ya kimataifa kama shirika la wakimbizi - UNHCR kwa ajili ya miradi ya misaada.

Ujerumani ndio mfadhili mkubwa wa Uganda baada ya Uingereza ambayo pia imesitisha ufadhili wake.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG