Maelfu ya watu walikufa katika mzozo wa miaka miwili, ambao ulimalizika rasmi Novemba mwaka jana. Pande zote mbili zimeshutumiana kwa ukatili, pamoja na mauaji ya watu wengi, ubakaji na kuwaweka watu kizuizini kiholela, lakini pande zote zilikana kuhusika na ukiukaji wa kimfumo.
"Utiaji saini wa makubaliano huenda huenda kwa kiasi kikubwa ulisitisha milio ya bunduki, lakini haukusuluhisha mzozo ulioko kaskazini mwa nchi hiyo, hususani huko Tigray, na wala huijaleta amani kamili," mwenyekiti wa Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Binadamu kwa Ethiopia Mohamed Chande Othman, alisema katika taarifa iliyoambatana na ripoti hiyo.
Katika ripoti yake, Tume imesema ukiukwaji wa haki za binadamu huko Tigray ulikuwa “mkubwa sana na unaoendelea," na kusema kumekuwepo na mashambulizi yaliyofanywa na Jeshi la Ulinzi la Eritrea (EDF) dhidi ya raia.
Eritrea, ambayo ilipeleka wanajeshi kupigana bega kwa bega na jeshi la serikali ya Ethiopia wakati wa mzozo huo, imekana shutuma kutoka kwa wakaazi na vikundi vya kutetea haki kwamba wanajeshi wake walihusika na ukiukaji huko Tigray.
Katika maoni yake kwa shirika la habari la Reuters, waziri wa habari wa Eritrea Yemane Ghebremeskel alielezea ugunduzi wa ripoti hiyo kuwa ni ya kashfa na kusema kuwa nchi yake ilikuwa inaandaa majibu rasmi.
Jeshi la Ethiopia na wasemaji wa serikali hawakujibu maombi kutoa maoni yao juu ya ripoti hiyo.
Forum