Muungano wa vyama vitatu vya upinzani uliitisha mandamano dhidi ya utawala wa muda wa mkoa huo unao ongozwa na Tigray People’s Libetation Front (TPLF), ambalo limeongoza siasa za Ethiopia kwa karibu miongo mitatu mpaka mwaka 2018.
Hailu Kebebe afisa mwandamizi wa chama cha Salsay Weyane Tigray, ameiambia AFP kwamba vikosi vya usalama vimezuia maandamano kwa kukamata na kupiga wafusai.
Amesema polisi iliwakamata watu takriban 26 toka Jumatano ikijumuisha Hayalu Godefay mwenyekiti wa chama na Dejen Mezgebe, rais wa chama cha Tigray Independent Party – TIP.
Forum