Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:24

Misri, Ethiopia na Sudan waanza tena mazungumzo kuhusu bwawa la Ethiopia


Picha ya bwawa la Grand Ethiopian Renaissance, Guba, Ethiopia, July 21, 2020.
Picha ya bwawa la Grand Ethiopian Renaissance, Guba, Ethiopia, July 21, 2020.

Misri, Ethiopia na Sudan Jumapili wameanza tena mazungmzo ambayo yamekuwepo kwa miaka kadhaa kuhusiana na bwawa lenye utata lililojengwa na Ethiopia kwenye mto Nile.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, mazungumzo hayo yamerejelewa baada ya rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kusema mwezi uliopita kwamba wanalenga kufikia makubaliano ndani ya miezi 4, kuhusu operesheni za bwawa hilo la Ethiopia Renaissance lililogharimu dola bilioni 4.6 za kimarekani na lililopo kwenye mto wa Blue Nile.

Blue Nile unakutana na White Nile karibu na mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kabla ya kuendelea upande wa kaskazini kuelekea Misri, na hatimaye kwenye bahari ya Mediterranean. Misri inahofia kwamba bwawa hilo huenda likaathiri shughuli zake iwapo litaendeshwa bila kuzingatia maslahi yake.

Taifa hilo la kiarabu lenye idadi kubwa zaidi ya wakazi hutegemea maji ya Nile kwa ajili ya kilimo, ambapo chanzo cha asilimia 85 ya maji yake ni Ethiopia.

Forum

XS
SM
MD
LG