Moto huo umewalazimisha wakuu wa miji kuwahamisha wakazi wa vijiji vinane na hospitali moja wakati wafanyakazi wa zima moto wakipambana na mioto inayoendelea kuwaka katika sehemu mbali mbali za taifa hilo.
Upepo mkali na viwango vya juu vya joto katika majira haya ya kiangazi yanazuia juhudi za mamia ya zima moto kuendelea na kazi zao licha ya kusaidiwa na ndege zinazomwaga maji kujaribu kuzima mioto hiyo.
Kiwango cha juu cha tahadhari kutokana na moto katika wilaya nyingi za nchi hiyo kimetangazwa ikiwa ni pamoja na sehemu kubwa ya mji mkuu wa Athena kwa siku ya pili mfululizo hii leo.
Maafisa wamepiga marufuku watu kutembelea maeneo ya milimani na misitu katika wilaya hizo hadi angalau kesho Jumatano.
Chanzo cha habari hii ni mashirika mbalimbali ya habari.
Forum