Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:36

Mioto ya msituni yauwa watu 6 Hawaii


Moshi na miali ya moto kutoka kwenye moto wa nyikani umetanda katikati mwa jiji la Lahaina, huko Maui, Hawaii, Jumanne, Agosti 8, 2023. (Picha na Alan Dickar kupitia AP)

Moto huo ulienea katika Mji wa Lahaina ikiwa ni pamoja na Mtaa wa Front, eneo maarufu la maduka na migahawa msemaji wa Kaunti ya Maui Mahina Martin alisema

Mioto ya msituni ambayo imeharibu sehemu za kisiwa cha Hawaii cha Maui imeua watu 6 maafisa walisema siku ya Jumatano.

Richard Bissen Jr Meya wa jumuiya ya Maui Magharibi ya Jiji la Lahaina alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba pia wamehamisha watu mara 13 kwa sababu ya mioto mitatu. Moto huo ulienea katika Mji wa Lahaina ikiwa ni pamoja na Mtaa wa Front, eneo maarufu la maduka na migahawa msemaji wa Kaunti ya Maui Mahina Martin alisema kwa njia ya simu mapema Jumatano.

Takriban watu 22 walijeruhiwa na moto huo wakiwemo kadhaa ambao walisafirishwa kwenda Honolulu kwa matibabu.

Forum

XS
SM
MD
LG