Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:28

Wanajeshi wa Canada kusaidia katika kudhibiti moto unaendela nchini


Moto ukiteketeza msitu nchini Canada

Wanajeshi wa Canada Jumapili wamepelekwa kaskazini mwa taifa hilo ili kukabiliana na mioto ya msituni jamii kadhaa za ndani ambako wakazi wamekimbia mioto inayowaka.

Jimbo la British Columbia lililopo karibu na bahari ya Pacific linajiandaa kwa wimbi la joto kali ambalo huenda likachochea zaidi moto unaoendelea kuwaka. Waziri wa Ulinzi wa Canada Bill Bliar kupitia ujumbe wakwa kwenye mtandao wa X, uliokuwa unajulikana kama Twitter amesema kwambawako pamoja na watu wa maeneo ya Kaksazini magharibi mwa nchi wakati wakikabiliana na moto huo.

Ameongeza kusema kwamba jeshi lililotumwa litasaidia katika kuuzima moto, kusafirisha watu, pamoja na kupanga mikakati mingine ya kudhibiti hali. Idadi kamili ya wanajeshi waliotumwa haijatolewa ingawa mamia wengine walitumwa awali kwenye majimbo mengine manne katika miezi ya karibuni, ili kukabiliana na moto, wakishirikiana na karibu zimamoto 11,000, wakiwemo 5,000 kutoka mataifa ya kigeni.

Forum

XS
SM
MD
LG