Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:40

Twitter yakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama Ufaransa juu ya kauli za chuki


FILE - Picha iliyopigwa Oct. 26, 2020, inaonyesha nembo ya Twitter katika simu ya Smartphone na tablet huko, Toulouse, Ufaransa.
FILE - Picha iliyopigwa Oct. 26, 2020, inaonyesha nembo ya Twitter katika simu ya Smartphone na tablet huko, Toulouse, Ufaransa.

Kampuni ya Twitter imekata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya Ufaransa iliyoamrisha kuwa iwape wanaharakati fursa kamili kupata nyaraka zake zote zinazohusiana na juhudi za kupambana na kauli za chuki, mawakili na vyanzo vya mahakama vimesema Jumamosi.

Mwezi Julai, Mahakama moja nchini Ufaransa iliamuru Twitter kuviruhusu vikundi sita vya Ufaransa vyenye kupinga ubaguzi kufikia nyaraka zote zinazohusiana na juhudi za kampuni hiyo katika kupambana na kauli za chuki tangu mwezi Mei mwaka 2020. Uamuzi huo ulihusisha operesheni za Twitter ulimwenguni, siyo tu Ufaransa.

Twitter imekata rufaa dhidi ya uamuzi huo na kesi imepangwa kusikilizwa Disemba 9, 2021, chanzo cha mahakama kimeliambia shirika la habari la AFP, ikithibitisha taarifa iliyotolewa na mawakili wa kikundi hicho.

Kampuni ya Twitter na mawakili wake walikataa kutoa maoni.

Amri hiyo ya Julai imesema kuwa Twitter ni lazima ikabidhi “nyaraka zote za kiutawala, mkataba, ufundi na biashara” ikionyesha rasilmali ilizotenga kwa ajili ya kupambana na chuki dhidi ya mahusiano ya jinsia moja, ubaguzi na mfumo dume kwenye tovuti, pamoja na makosa ya “kuruhusu uhalifu dhidi ya ubinadamu”.

Pia imesema Twitter ni lazima ionyeshe ni waratibu wangapi imeajiri nchini Ufaransa kuhakiki habari zilizoainishwa kuwa ni za chuki, na takwimu katika mchakato wa habari hizo.

Uamuzi wa mwezi Julai umeipa kampuni hiyo yenye makao yake San Francisco miezi miwili kutii amri. Twitter inaweza kuomba kusitishwa hilo ikisubiri rufaa.

Makundi hayo sita yanayo pinga ubaguzi yaliipeleka Twitter mahakamani nchini Ufaransa mwaka 2020, wakiituhumu kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa jamii ya Marekani kushindwa “kwa muda mrefu” kuzuia maoni ya chuki kutoka katika kurasa zake.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG