Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 14:34

Wanajeshi wa Guinea kuitisha kikao maalum cha baraza la mawaziri baada ya mapinduzi


Kifaru cha jeshi chapiga doria kwenye mitaa ya mji mkuu wa Guinea wa Conakry
Kifaru cha jeshi chapiga doria kwenye mitaa ya mji mkuu wa Guinea wa Conakry

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres, Jumapili amelaani kile kinachotajwa kama mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea, na kuwasihi wanajeshi waliosema  wamefanya mapinduzi hayo na kuchukua madaraka, kumuachilia huru rais Alpha Conde.

Guterres ameandika kwenye twitter “ Mimi binafsi nafuatilia kwa karibu sana hali inayojiri Guinea. Nalaani vikali kuiondoa serikali kwa nguvu za bunduki na ninatoa wito kwa kumuachilia mara moja rais Alpfa Conde”.

Vikosi maalumu vilivyochukua madaraka na kumkamata rais Conde, vimetangaza amri ya kutotoka nje usiku nchini kote, hadi itakapotolewa taarifa nyingine, na nyadhifa zote za magavana kuchukuliwa na jeshi.

Kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi limesema pia katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa kwamba, litaitisha baraza la mawaziri la serikali ya Conde na maafisa wengine wa ngazi juu saa tano asubuhi majira ya huko.

Katika ngome ya upinzani ya Bambeto mjini Conakry, wakazi na wanaharakati wa upinzani waliingia barabarani kwa wingi kusherekea wakati wanajeshi waliofanya mapinduzi wakisema kwamba wamemkamata rais.

XS
SM
MD
LG