Mafuriko hayo yalitokana na mvua kubwa ambayo ilisomba nyumba na barabara za vijijini, maafisa wamesema.
Wakazi waliliambia shirika la Habari la AP kuwa ilikuwa ni tukio baya kushuhudia kutokana na wingi wa maji yaliyokuwa yanaingia ndani.
Miongoni mwa miili ya watu waliokufa iliyopatikana ni ya watoto wadogo ambao walisombwa na maji .
Gavana wa Tennessee Bill Lee aliandika katika mtandao wa Twitter jana akiwasihi wakazi kuwa waangalifu na katika hali ya tahadhari kubwa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua nyingi.
Amesema wanafanyakazi kwa karibu sana na huduma za dharura pamoja na maafisa wa idara mbalimbali kuhakikisha usalama wa watu.