Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 04, 2023 Local time: 04:47

Marekani ina wasi wasi kwa wanahabari kunyanyaswa huko China


Mfano wa picha za wanahabari wanapokuwa kazini

Matamshi yake yalikuja chini ya saa 24 baada ya Beijing, kuishutumu BBC kwa kutangaza habari za uongo, juu ya mafuriko mabaya ya wiki iliyopita katika jimbo la kati la Henan na wakati mtangazaji huyo wa Uingereza aliposema wanahabari wake walikuwa wamenyanyaswa

Marekani ina wasi wasi sana juu ya unyanyasaji na vitisho kwa waandishi wa Habari wa kigeni wanaoripoti mafuriko yaliyosababisha vifo huko China, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, alisema Alhamis.

Matamshi yake yalikuja chini ya saa 24 baada ya Beijing, kuishutumu BBC kwa kutangaza habari za uongo, juu ya mafuriko mabaya ya wiki iliyopita katika jimbo la kati la Henan na wakati mtangazaji huyo wa Uingereza aliposema wanahabari wake walikuwa wamenyanyaswa.

Marekani ina wasi wasi mkubwa na ongezeko la unyanyasaji na vitisho kwa waandishi wa Habari wa Marekani na wengine wa kigeni huko Jamhuri ya watu wa China (PRC) pamoja na waandishi wa habari wa kigeni wanaoelezea uharibifu na vifo vilivyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni huko Henan, ilisema taarifa ya msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Ned Price.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG