Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:11

Mafuriko yasababisha maafa China


Wafanyakazi wa misaada wapeleka bidhaa kwa watu walioathiriwa na mafuriko China
Wafanyakazi wa misaada wapeleka bidhaa kwa watu walioathiriwa na mafuriko China

Wataalam wa hali ya hewa wamesema Jumatano kwamba takriban watu 25 wamekufa kutokana na mafuriko kwenye jimbo la Henan katikati mwa China kufuatia siku kadhaa za mvua, wakati wakitabiri kwamba mvua hizo zitaendelea kunyesha kwa siku tatu zaidi.

Ripoti zinasema kuwa barabara za mji mkuu wa jimbo hilo wa Zhengzhou zimesombwa maji wakati madereva wakilazimika kutembea kwa miguu huku maji yakiwafika kiunoni. Mafuriko hayo pia yanasemekana kusomba njia za reli ambazo zinategemewa kwa usafiri na watu wengi.

Watu 12 wanasemekana kufa kwenye vituo vya treni vya chini ya ardhi wakati takriban 500 waliokolewa kulingana na chombo cha habari cha serikali.

Mabwawa pamoja na hifadhi nyingine za maji zinasemekana kujaa kutokana na mafuriko hayo wakati kukiwa na wasi wasi wa kuporomoka kwa bwawa la Yihetan lililoko karibu na mji wa Louyang.

Tayari zaidi ya watu 100,000 wamepelekwa kwenye maeneo salama, wakati wanajeshi pamoja na polisi wakisaidia kupeleka misaada ya kibinadamu kwa watu walioathiriwa

XS
SM
MD
LG