Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:13

Trump : 'Kiongozi wa Islamic State Baghdadi ameuawa'


 Abubakr al Baghdadi
Abubakr al Baghdadi

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa kiongozi wa Islamic State, Abu Bakr al-Baghdadi ameuawa.

Trump amesema Baghdadi alijilipua baada ya kujikuta amezungukwa na majeshi maalum ya Marekani.

Rais ameshukuru nchi zote zilizotoa msaada katika operesheni hiyo ikiwemo Russia, Uturuki, Iraqi na washirika wa Marekani, Wakurdi.

Trump amesema Marekani itaendelea kuhakikisha inakimaliza kikundi hiki na kukitokomeza kabisa.

Amesema Jeshi la Marekani limefanya operesheni nchini Syria, ambalo limemuua kiongozi katika operesheni iliyokuwa hatari sana, na wengi katika wafuasi wake waliuawa. Lakini Marekani haikupoteza raia wake yoyote.

Russia amesema ilitoa msaada mkubwa wa kijeshi na Iraq katika opereshini hiyo, iliyokuwa na mafanikio makubwa.

"Baghdadi amekufa kama mbwa na amekufa kifo cha mtu muoga," Trump amesema.

Trump alituma ujumbe wa tweet jioni Jumamosi : “Kitu kikubwa kimetokea punde hivi!”

Taarifa ya vyombo vya habari imesema shambulio hilo lilimkusudia Baghdadi aliyekuwa katika jimbo la Idlib Syria, katika operesheni iliyohusisha ndege aina ya helikopta, ndege za kivita na ndege sizisokuwa na rubani.

Mnamo Julai ripoti ya UN ilitoa ilani kuwa viongozi wa juu wa Islamic State “ ni kati ya wale waliofanikiwa kuingia eneo la Idlib.”

Baghdad mara kadhaa ameripotiwa kuwa ameuawa wakati ilikuwa siyo kweli.

Ujumbe wake wa mwisho uliokuwa umerikodiwa katika sauti ulitolewa mwezi Septemba, ambapo aliahidi vita dhidi ya Marekani na washirika wake haitamalizika.

XS
SM
MD
LG