Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:24

Syria : Wakazi waomboleza wakati vita ikiendelea baada ya suluhu kushindikana


Waasi wa Syria wanaosaidia na Uturuki wakiwa mpakani mwa Tal Abyad, Syria, Oct. 17, 2019.
Waasi wa Syria wanaosaidia na Uturuki wakiwa mpakani mwa Tal Abyad, Syria, Oct. 17, 2019.

Kipindi cha kusheherekea kwa milio ya risasi kilitanda katika anga kama vile ni fataki zilizorushwa angani katika miji ya kaskazini mashariki mwa Syria Alhamisi usiku, lakini Ijumaa mchana hali ilikuwa kimpya zaidi.

Masharti ya kusitisha mapigano kwa siku tano yalikuwa sasa yako wazi. Kusitisha kwa Uturuki kufanya mashambulizi kulikuwa kunategemea hatua ya vikosi vya ukombozi vya Syria vinavyoongozwa na Wakurdi kurudi nyuma kutoka mpakani, kitu ambacho SDF imesema haitofanya hivyo.

Ijumaa jioni, SDF ilitoa tamko kutangaza kuwa usitishaji wa mapigano umeshindikana.

“Mashambulizi ya bunduki, vifaru na silaha nzito pamoja na mashambulizi ya anga yaliendelea bila ya kusita,” limesema tamko hilo. “kwa ajili ya haki ya kujihama, wapiganaji wa SDF walijibu mashambulizi yote hayo.

Taarifa za awali juu ya kupigwa mabomu na mapigano katika miji ya mpakani baadae yalithibitishwa wakati majeruhi walipowasili hospitali nje ya eneo la mapigano.

Sokoni eneo la Qamishli, mji ulioko katika mpaka wa Syria na Uturuki ambao umepigwa mabomu mara kadhaa, wakazi wamesema hawataki SDF iache kupigana.

Wamepoteza watu wengi wakipigana na wapiganaji wa kikundi cha Islamic State, amesema Mohammed, 32, mzazi wa vijana wawili.

Lakini vita hii imesaidia kuongeza eneo ambalo linasimamiwa na Wakurdi kwa hali zote kwa masafa na nguvu.

"Tayari tumelipa thamani kubwa kwa kuuawa watu wengi," amesema, akiegemea meza ya biashara ya familia yake yenye mbogamboga kama vile biringanya, viazi ulaya na malimao.

Mpwa wake Mahmoud, mwenye umri wa miaka 11, alikuwa akitabasamu akiwa na haya huku akiongea. Alisema kati ya waliouawa ni Mohammed kijana mwenye umri wa miaka 13, rafiki yake na wakicheza mpira siku zote pamoja.

"Niliongopa," amesema kimyakimya. "Bomu lilikuja upande wetu."

Pia mashambulio ya mizinga na bunduki yaliendelea Ijumaa siku moja baada ya kufikiwa makubaliano kati ya Marekani na Uturuki baada ya Rais Tayyip Erdogan kukubali kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano.

Milio ya bunduki za rashasha na mizinga ilisikika katika mji wa mpakani wa Ras al Ain huku mosi ukatanda katika sehemu moja ya mji nhuo wa Syria.

Makubaliano ya kusitishwa mapigano yalitangazwa na makamu rais wa marekani Mike Pense baada ya mazungumzo mjini Ankara na rais Erdogan na kusifiwa na rais Donald Trump kama makubaliano muhimu yatakayo okoa maisha ya mamilioni ya watu.

Lakini muda mchache baadae uturki ilidai kwamba hawakukubaliana usitishaji mapigano bali wamekubali kusitisha kwa muda wa siku 5 ili kuwaruhusu wapiganaji wa kikurdi kuondoka kukoka ukanda wa kilomita 30 kwenye mpaka wa wa Syria.

Haifahamiki wazi hivi sasa iwapo wapiganaji wa kikurdi wa kundi la SDF watakubali kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo.

XS
SM
MD
LG