Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:48

Uturuki yaanza kupokea silaha kutoka Russia


Ndege ya mizigo ya Russia ikiwasili na shehena ya sehemu ya mfumo wa silaha za ulinzi wa aina ya S-400, Ankara, Turkey, Ijumaa Julai 12, 2019.
Ndege ya mizigo ya Russia ikiwasili na shehena ya sehemu ya mfumo wa silaha za ulinzi wa aina ya S-400, Ankara, Turkey, Ijumaa Julai 12, 2019.

Wizara ya ulinzi ya Uturuki imetangaza kuwasili kwa sehemu ya kwanza ya shehena ya mfumo wa silaha za ulinzi wa anga aina ya S-400, kutoka Russia.

Ndege ya mizigo ya Russia, iliwasili ikiwa imebeba shehena ya mfumo wa silaha hizo katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Murted, Ankara.

Silaha hizo kutoka Russia, za kwanza kuuzwa kwa mwanachama wa Umoja wa Kujihami wa Ulaya, Nato, imesababisha wasiwasi kwamba Uturuki inakaribia ushawishi wa Moscow.

Uturuki ilikuwa imekataa kuzingatia masharti ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba huo, ulioripotiwa kugharimu zaidi ya dola bilioni 2.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Washington, DC

XS
SM
MD
LG