Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 02, 2023 Local time: 17:14

Serikali ya Syria inashutumiwa kutofungua fursa za msaada wa kibinadamu


Mapigano yanayoendelea huko Syria ambayo yamesababisha uharibifu wa nyumba katika baadhi ya majimbo nchini humo

Mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia pamoja na utawala wa Syria yameharibu takribani maeneo yote huko kaskazini mwa Hama na kusini mwa jimbo la Idlib na kuwakosesha makazi watu 800,000 waliopo kwenye mpaka kati ya Syria na Uturuki

Taasisi inayofuatilia masuala ya vita na haki za binadamu nchini Syria yenye makao yake Uingereza iliieleza VOA kwamba Serikali ya Syria haijafungua fursa ya msaada wa kibinadamu kwa raia katika jimbo la Idlib huko kaskazini magharibi mwa Syria, ngome ya mwisho ya makundi ya waasi.

Taasisi ya Syrian Observatory for Human Rights inaandika ukiukaji wa haki za binadamu huko Syria ikieleza kuwa tangazo la utawala la kufungua fursa ya msaada wa kibinadamu ni uongo na kwamba hakuna raia aliyeachwa katika eneo ambapo raia wote tayari wameondoka kutokana na mapigano yanayofanywa na vikosi vya utawala.

Rami Abdulrahman mkuu wa taasisi hiyo inayofuatilia masuala ya kibinadamu aliiambia Sauti ya Amerika- VOA kuwa njia hiyo imewekwa na Russia na utawala wa Syria kwa ajili ya vyombo vya habari kusema kwamba raia wanakimbia kuelekea maeneo yanayodhibitiwa na utawala wa Syria.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG